Uzuri ni kwamba hakuna kitu chochote hapa duniani ambacho biblia haijazungumzia. Sasa hupaswi kweli kusikiliza maneno ya watu lakini unapaswa kuangalia neno la Mungu je, linaongea nini juu ya haya nayoambiwa na hawa wanadamu. Wale unaowaona ni watu wasio na akili na waovu ndiyo hao hao wanaokuambia ukweli juu ya mwenza wako. Mshitaki wetu sisi ni shetani naye anazunguka zunguka akitafuta mtu ammeze. MANENO YA MWANADAMU YANAKUWA HAYANA NGUVU ENDAPO YANAPINGANA NA MANENO YA MUNGU. Kama unasemwa na watu na hujapata kibali kwao usije ukajitia kiburi kwa kusema eti mimi simsikilizi mwanadamu na wakati huo hata Mungu hujamsikiliza wala humsikilizi pia. Ili uheshimike na upate kibali kwa Mungu na kwa wanadamu ni lazima umtumaini Bwana. Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,Wala usizitegemee akili zako mwenyewe Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Kama mwanamke amchaye Bwana ndiye atakayesifiwa wewe unaelewa nini unapomuona mchumba wako anakuwa kipingamizi katika mambo yanayomhusu Mungu? Kama ukipambana na uzuri na kuushikilia ujue ni lazima wewe utashindwa maana uzuri utakushinda na utakuacha na kuufuata uzee. Uzuri huwa unapita maana hii miili yetu inaharibika lakini roho haipiti wala haizeeki ndiyo maana neno linasema kwamba mwanamke amchaye Bwana ndiye atakayesifiwa. Ubatili ni jambo lisilodumu na la kupita. Nasisitiza kwamba ule uzuri wake kisije kikawa ndicho kigezo cha wewe kumfanya kuwa mke. Uzuri ni ubaliti lakini haimaanishi usiwe na mwanamke mzuri anaekupendeza, ila tu ule uzuri wake kisiwe ni kigezo cha yeye kuwa mke wako. Huo ni upendeleo lakini biblia inakuambia kwamba hudanganya. Sasa usije ukampenda msichana kwa upendeleo yani unamuona kabisa hana sifa za kuitwa mke halafu wewe ukamfanya kuwa mke. Hivyo ulivyo wewe ni kwa neema tu siyo kwamba unastahili sana au una point yoyote ya kumwambia Mungu kwamba ulistahili uwe hivyo. Kwa mfano sisi tulio ndani ya Kristo tumeokolewa kwa neema na siyo kwamba tulistahili sana. Upendeleo unaozungumziwa hapa ni ile hali ya kufanya kitu kwa mtu asiyestahili. Hapa ndiko penye upofu mwingine hasa kwa wanaume wengi. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Watu wengi wanapenda kuangalia kwa akili zao wenyewe na hata wanapoona kabisa mambo siyo mazuri katika hayo mahusiano huwa wanajifanya hawaoni kwaajili ya kulinda maslahi yao binafsi waliyoyaona kwa huyo mtu pengine ni muonekano, fedha au mali alizo nazo. Mungu wa dunia hii ambaye ni shetani anapopofusha fikra zako basi hutataka kabisa kumtazama yeye kupitia neno la Mungu kwamba linasemaje juu yake. Kama injili ilisitirika kwako ukaiweka pembeni basi ujue ulipotea njia katika hayo mahusiano. Kama hujamtazama kwa kutumia neno la Mungu basi hesabu maumivu kabisa katika hiyo ndoa. Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea Īmbao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Ili usiendelee kumtafuta gizani katika hali ya upofu ni lazima upate nuru katika macho yako ambayo hiyo nuru hutaipata kwa marafiki, ndugu wala wazazi wako bali utaipata kupitia neno la Mungu tu na ukijifanya mjuaji utakuja kujuzwa uliyopaswa kuyajuwa kabla hujachukua maamuzi yako na kumuoa au kuolewa naye. Katika kumtazama mtu sahihi katika maisha yako unaweza ukatazama kwa macho ya kawaida ukachanganya na maoni ya watu wengine na wote wakakupongeza lakini kumbe umepigwa upofu. Naomba leo tujifunze juu ya kumpata mtu sahihi katika maisha kwa wale wanaotamani sana kuwa na mahusiano bora katika ndoa zao.
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorWrite something about yourself. No need to be fancy, just an overview. ArchivesCategories |